Kampuni ya Huawei inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulimwenguni, leo imezindua programu ya elimu inayoitwa Seeds for the Future hapa nchini Tanzania.
Programu ya ‘Seeds for the Future’ inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa hapa nchini kutoka vyuo vikuu kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China.
Mradi huo umelenga kuwa kusaidia kile kinachofundishwa shuleni kukidhi mahitaji halisi ya soko la ajira kwa vijana hapa nchini ikiwa ni pamoja na kupanua uelewa wa TEHAMA na kuhamasisha ushiriki katika sekta hii ili kuendana na jamii ya sasa teknolojia ya habari na mawasilino.
Akizunguma wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliochaguliwa kusoma China, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Bruce Zhang alisema ni wazi kwamba wanafunzi hawa watapewa kipaumbele kwenye fursa za kujifunza kupitia kujumuika na wafanyakazi wa Huawei na kutembelea maabara ya kampuni hiyo ambako wataweza kuona na kufanya majaribio ya teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni